Tuesday, 21 May 2024
SUZAN KUNAMBI ATEULIWA KUWA KATIBU MKUU UWT
Saturday, 4 May 2024
CHATANDA ASHIRIKI MAZISHI YA ALIYEKUWA MWENYEKITI UWT SENGEREMA, JANE MSOGA
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) (kushoto) akiwa kwenye ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Umoja wa Wanawake Wilaya ya Sengerema Ndg. Jane James Msoga iliyofanyika Mei 3, 2024 katika Kanisa la AICT (African Inland Church Of Tanzania)
..............................
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) amefika Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza katika Kanisa la AICT (African Inland Church Of Tanzania) kwaajili ya kushiriki Ibada ya Mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti Umoja wa Wanawake Wilaya ya Sengerema Ndg. Jane James Msoga ambaye alifariki Dunia tarehe 30.04.2024 Katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Seko Toure.
Mwenyekiti Chatanda akiwa Sengerema amepokelewa na viongozi wa Chama na Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Bi. Senyi Ngaga na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Wajumbe Kamati ya Siasa Wilaya, Wenyeviti wa UWT Wilaya sita za Mwanza.
Marehemu Jane ameacha Mume na Watoto 11 wakiwemo watoto wakike 7 na Wakiume 4. Mwili wake unatarajia kuhifadhiwa katika nyumba yake ya Milele Sengerema Mjini Kata ya Nyampurukano Mei 3, 2024.
Mazishi hayo upande wa Serikali
yameongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndg. Said Mtanda na kuhudhuriwa na Wakuu
wa Wilaya Sengerema na Misungwi, Mjumbe Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Viti 20
Tanzania Bara Ndg. Ellen Bogohe, Mwenyekiti CCM Sengerema, viongozi wa UWT Mkoa
wa Shinyanga, Wajumbe Baraza Kuu UWT Taifa, Mbunge Jimbo la Buchosa na
Sengerema, Wabunge Viti Maalum Mkoa wa Mwanza. 
Thursday, 25 April 2024
RAIS DKT. MWINYI AKOSHWA NA MDAHALO WA WANAWAKE NA MUUNGANO, AIPONGEZA UWT.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akiwa na Mkewe Mama Mariam Mwinyi wakiwasilimia Viongozi wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) walipowasili katika ukumbi wa mkutano wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya kulifungua Kongamano la Wanawake na Muungano lililofanyika leo 25-4-2024.(Picha na Ikulu)
...........................
Na Mwandishi Wetu
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi
ameipongeza Jumuiya ya Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa kazi
kubwa waliyoifanya kuwaletea maendeleo wanawake na kukiimarisha Chama Cha
Mapinduzi (CCM) pamoja na kuandaa mdahalo wa wanawake na Muungano.
Pia,
ameupongeza umoja huo kwa kuendelea kuwa kinara katika kubuni na kutengeneza
mambo mbalimbali yenye lengo la kuimarisha CCM, kikiunganisha na wananchi na
kuimarisha umoja na mshikamano na wananchi.
Dkt. Mwinyi amesema hayo jijini Dar es Salaam leo
Aprili 25, 2024 alipofungua mdahalo wa kitaifa wa Wanawake na Muungano
uliondaliwa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) na kufanyika katika ukumbi wa
Mlimani City.
Mdahalo huo uliohudhuriwa na viongozi mbalimbali
wakiwemo wake za viongozi wakuu
wastaafu, mawaziri, naibu mawaziri, wabunge, wawakilishi, wananchi na wanachama
wa jumuiya hiyo na wa CCM.
Kwa upande wake mwenyekiti wa UWT Taifa Ndg. Mary
Pius Chatanda amesema wanafanya mdahalo wa kuelekea miaka 60 ya Muungano na
kujadili nafasi ya mwanamke katika kipindi cha nyuma,sasa na kijacho
Kwa upande wake, Makamu Mwenyekiti wa UWT,
Ndg.Zainab Shomari amesema muungano huo uliletwa na nchi mbili za Tanganyika na
Zanzibar zikiwa huru, haukuwa wa kuchanganya mchanga tu, bali wa kidamu kwa kuwa Zanzibar kuna watu wa makabila
mbalimbali.
Washiriki wa Kongamano la Wanawake na Muungano
kuadhimisha Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililofanyika leo
25-4-2024 katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam, wakimsikiliza
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi
akihutubia na kulifungua Kongamano hilo.(Picha na Ikulu)
MKE wa Rais wa Zanzibar Mama Mariam Mwinyi akiwa
na Wake wa Viongozi wakifuatilia hutuba ya ufunguzi wa Kongamano la Wanawake na
Muungano kuadhimisha Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi
akifungua Kongamano hilo lililofanyika leo 25-4-2024 katika ukumbi wa Mlimani
City Jijini Dar es Salaam.(Picha na Ikulu)
WASHIRIKI wa Kongamano na Wanawake na Muungano
kuadhimisha Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakishingilia wakati
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi
akihutubia na kulifungua Kongamano hilo lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani
City Jijini Dar es Salaam leo 25-4-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akimkabidhi Zawadi Maalum ya Picha
iliyotolewa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa Rais wa Jamhuri wa Muungano
wa Tanzania Mhe.Dkt,Samia Suluhu Hassan, akipokewa kwa niaba Mhe.Wanu Hafidh
Ameir, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Wanawake na Muungano
lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam leo
25-4-2024.(Picha na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi,akimkabidhi Zawadi Maalum ya Picha
iliyotolewa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mjane wa Rais wa Kwanza wa
Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Hayati Sheikh Abeid Amani Karume
Mama Fatma Karume,wakati wa ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Wanawake na
Muungano lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam leo 25-4-2024.(Picha
na Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, akimkabidhiwa Zawadi Maalum ya Picha
iliyotolewa na Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) kwa mchango wake, akikabidhiwa
na Mwenyekiti wa UWT Taifa Mary Chatanda, wakati wa ufunguzi wa Kongamano la
Kitaifa la Wanawake na Muungano
kuadhimisha Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lililofanyika
katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam leo 25-4-2024.(Picha na
Ikulu)
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi akihutubia na kulifungua Kongamano la
Kitaifa la Wanawake na Muungano kuadhimisha Miaka 60 ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania,i lililofanyika katika ukumbi wa Mlimani City Jijini Dar es Salaam leo
25-4-2024.(Picha na Ikulu)
VIONGOZI Wastaafu wa UWT wakifuatilia hutuba ya
ufunguzi wa Kongamano la Kitaifa la Wanawake na Muungano lililofanyika leo
25-4-2024 na kufunguliwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Mhe.Dk.Hussein Ali Mwinyi, lililofanyika katika ukumbi wa Mlomani
City Jijini Dar es Salaam leo 25-4-2024.(Picha na Ikulu)
Wednesday, 24 April 2024
UWT YAMPONGEZA MKE WA WAZIRI MKUU MSTAAFU MALECELA KWA MALEZI BORA KWA MME WAKE
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda (MCC) amemshukuru Mungu kwa kumjaalia afya na umri mrefu Waziri Mkuu mstaafu Dkt John Samwel Malecela sambamba na kumpongeza Mama Anne Malecela kwa kuwajibika vyema na kumuhudumia mumewe.
Mwenyekiti Chatanda aliyasema hayo Aprili 21, 2024 wakati wa hafla ya kumpongeza Dkt. John Samwel Malecela kwa kutimiza miaka 90 ya kuzaliwa kwake ambapo Mgeni rasmi wa hafla hiyo alikuwa Dkt Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.
Aidha Chatanda , Mary Chatanda , amempongeza Mke wa Waziri Mkuu Mstaafu Anne Kilango Malecela kwa matunzo na malezi mazuri kwa Mume wake Dkt. John Samwel Malecela ambaye ameendelea kuwa na afya na siha njema.
"Tunakupongeza Mama Yetu Anna Kilango Malecela kwa kumtunza vizuri mume wako ambaye amelitumikia Taifa ili kwa uzalendo mkubwa katika ngazi mbalimbali," alisema Chatanda.

MWENYEKITI UWT TAIFA ALIVYOWAFARIJI WAFIWA , WAATHIRIKA WA MAFURIKO IFAKARA
Chatanda akikabidhi pole hiyo kwa waathirika
Pole hiyo ikitolewa.
Pole ikitolewa.
Chatanda akizungumza na waathirika hao.
MDAHALO WA KITAIFA WA WANAWAKE NA MUUNGANO KUFANYIKA KESHO MLIMANI CITY JIJINI DAR ES SALAAM
Rais wa Tanzania na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dkt. Samia Suluhu Hassan
...............................
Na Dotto Mwaibale
WAKATI tukielekea Maadhimisho ya
siku ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar yatakayofanyika Aprili 26, 2024,
Umoja wa Wanawake Tanzania ( UWT ) umeandaa mdahalo wa Kitaifa wenye Dhima ya
Nafasi ya Wanawake ndani ya miaka 60 ya Muungano. Tulipotoka, Tulipo na
Tunapoelekea litakalofanyika kesho Aprili 25, 2024 Ukumbi wa Mlimani City
Jijini Dar es Salaam.
Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja huo Mary Chatanda akizungumzia kuhusu mdahalo
huo alisema maandalizi yote yapo tayari na kuwa utakuwa na mada mbalimbali
zitakazo tolewa na wabobezi wa masuala ya kisiasa nchini ambapo mgeni rasmi
atakuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussen Ali
Mwinyi.
Chatanda aliwataja wabobezi hao ambao pia walishika nafasi za juu za
uongozi hapa nchini kuwa ni Profesa Palamagamba Kabudi ambaye atatoa mada
inayohusu Historia ya Nafasi ya Mwanamke katika Muungano na Balozi Amina Salum
Ali ambaye atatoa mada inayoelezea Mwanamke na uongozi, faida za Muungano
katika ukuaji wa kijinsia (kisiasa, kiuchumi na kijamii)
Aliwataja watoa mada wengine kuwa ni Mama Anna Abdallah ambaye ataelezea
mchango wa UWT katika Muungano, Profesa Ruth Meena ambaye atatoa mada
inayozungumzia matarajio ya miaka 60 ya Muungano, Nafasi ya mwanamke katika
uongozi, ambapo pia Mama Zakia Meghji na viongozi wengine maarufu na wastaafu
watakuwepo.
Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda ambaye ametajwa kuwa ni moto wa kuotea mbali usiozimika na timu yake ndio waliouandaa mdahalo huo anatumia nafasi hiyo kuwaalika wananchi kwenda kuhudhuria mdahalo huo ambao ni muhimu kwa muktaza wa Taifa letu la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kuwa litaanza Saa 2: 00 asubuhi.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania ( UWT ) Taifa, Mary Chatanda
Makamu Mwenyekiti wa UWT Taifa, Zainabu Shomari
Profesa Palamagamba Kabudi
Saturday, 20 April 2024
FALSAFA YA 4R YAMPATIA RAIS DKT. SAMIA SULUHU HASSAN, SHAHADA NYINGINE YA UDAKTARI
*Falsafa ya 4R yampatia Rais Samia shahada nyingine ya udaktari
*Baada ya India, chuo kingine kikuu kikubwa cha Uturuki chamtunuku Rais Samia shahada ya udaktari
................................
Na Mwandishi Wetu - Zanzibar
Huku wakiwa wameshika bango lenye kauli mbiu
maarufu ya "Songa na Samia," vijana wanaopiga mbizi kwa sarakasi
kwenye eneo la Forodhani la Zanzibar, wametoa video yao mpya kuchambua falsafa
ya 4R ya Rais Samia Suluhu Hassan kuelekea maadhimisho ya miaka 60 ya Muungano
wa Tanganyika na Zanzibar.
Siku chache baada ya vijana hao kutoa video yao
hiyo, Rais Samia ametunukiwa Shahada ya Heshima ya Udaktari (Honoris Causa) ya
Uchumi na Chuo Kikuu cha Ankara nchini Uturuki kwenye hafla iliyofanyika chuoni
hapo Ankara, Uturuki, leo tarehe 18 Aprili, 2024.
Mwezi Oktoba mwaka jana, Rais Samia alitunukiwa
shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa ya kielimu (Doctorate Honoris Causa)
na Chuo Kikuu cha Jawaharlal Nehru nchini India. huku akiendelea na ziara yake
nchini India.
Hadi sasa, Rais Samia ametunukiwa shahada za
heshima takribani 4 kutoka vyuo vikuu vikubwa ndani ya nje ya nchi ndani ya
miaka mitatu tu ya Urais wake.
Shahada hizo zinatambua jitihada kubwa
inayofanywa na Serikali yake kuleta mabadiliko katika mifumo ya kisiasa,
kiuchumi na katika sheria zetu za uchaguzi nchini.
Kwenye uongozi wake, Rais Samia anaamini katika
kile kinachojulikana kama 4R – ikiwa ni ufupisho wa maneno manne ya lugha ya
Kiingereza; Reconcilation (Maridhiano), Resilience (Ustahamiliivu), Reforms
(Mabadiliko) na Rebuidlding (Kujanga Upya).
Hizi ndiyo 4R za Rais Samia ambazo zimeleta
mafanikio makubwa kwenye uongozi wake tangu aingie madarakani Machi 19, 2021:
MARIDHIANO
Kwenye kujenga Tanzania bora,.Rais Samia amesema
kuwa anatamani kujenga jamii yenye maridhiano na maelewano. Anatamani kujenga
umoja pasipo kujali tofauti zetu za kisiasa, kidini, kikabila na nyingine zote.
Hili litawezekana kwa kujenga jamii inayopata
haki sawa mbele ya sheria, isiyobaguana
na inayotoa fursa sawa sawa za kiuchumi kwa wote.
Rais Samia anaamini kuwa maridhiano hayawezi
kupatikana penye ubaguzi na pale ambapo kuna wanaokosa fursa na haki zao za
kiuchumi na kiraia.
USTAHIMILIVU
Tanzania haiwezi kusonga mbele kama wananchi na
viongozi watakuwa legelege kulinda yaliyo yetu. Wahenga walisema Umoja ni Nguvu
na namna pekee ya kupambana na changamoto zote zinazoikumba dunia kwa sasa ni
kwetu sisi kufanya hivyo kwa Umoja na Mshikamano.
Huko tuendako tutatikiswa na kuyumbishwa. Iwe
kiuchumi, kimazingira, kijamii na kisiasa lakini ni lazima tujenge
ustahamivu," Rais Samia alisema.
Hii ni kwa sababu hakuna nchi nyingine zaidi ya
hii na hapa ndiyo kwetu. Nilitiwa nguvu sana na namna Watanzania walivyopokea
tukio la Royal Tour kwa uzalendo wa kipekee.
MABADILIKO
Kuna msemo mmoja maarufu kwamba kitu pekee cha
uhakika kwa mwanadamu ni mabadiliko.
Rais Samia amedhamiria kwamba serikali yake
itajitahidi kufanya mabadiliko katika mifumo ya kisiasa, kiuchumi na katika
sheria zetu za uchaguzi.
Lengo ni kwamba Tanzania iende na wakati na –
kama ilivyokuwa wakati mwingine, tujue mapema ni wakati gani wa kufanya jambo
hata kama si watu wanaliunga au hawaliungi mkono kwa wakati husika.
Mabadiliko katika sheria za uchaguzi yataleta
ushindani wa haki na kuwapa watu fursa ya kuwachagua wawatakao kuwaongoza.
Kwenye uchumi, mabadiliko yatakuwa na lengo la kutoa fursa zaidi kwa watu wengi
zaidi kunufaika kiuchumi badala ya wachache.
KUJENGA UPYA
"Ninafahamu kwamba wananchi hawali
maridhiano, ustahamivu wala mabadiliko," Rais Samia alisema.
Kama walivyofanya watangulizi wa Rais Samia,
lengo kuu linatakiwa kuwa ukuaji wa uchumi wa Tanzania. Uchumi utakaoongeza
ajira kwa vijana wetu na utakaofungua fursa kwa makundi yote ya kijamii yaliyo
nchini.
Tayari serikali inaendeleza miradi mikubwa ya
miundombinu na mengine kwenye sekta ya madini na nishati. Juhudi zilizofanywa
kupitia kampeni ya Royal Tour zina lengo la kuzimua sekta muhimu ya utalii
iliyoathiriwa sana na ugonjwa wa Covid 19. Katika kilimo serikali inafanya
mabadiliko makubwa ili sekta hiyo muhimu ianze kuwa na mchango inaostahili
kwenye uchumi wetu.
"Ninaamini kwamba kwa jitihada zetu za R nne, tutaweza kutimiza malengo ya kuwa na mfumo wa vyama vingi vya siasa. Lengo kuu halikuwa kuwa na vyama vingi vya siasa bali lengo lilikuwa kujenga jamii yenye uzalendo, maridhiano, ustahamivu na yenye uchumi unaokua kwa wote na endelevu," Rais Samia alisema.























.jpg)



.jpeg)
.jpeg)




