Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. John Samwel Malecela akizungumza kwenye hafla ya kutimiza miaka 90 tangu azaliwe iliyofanyika Kilimani nyumbani kwake jijini Dodoma Aprili 21, 2024. Kushoto ni mgeni rasmi wa hafla hiyo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa CC, Dkt. Hussein Ali Mwinyi.
.................................
Na Mwandishi Wetu, Dodoma
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda (MCC) amemshukuru Mungu kwa kumjaalia afya na umri mrefu Waziri Mkuu mstaafu Dkt John Samwel Malecela sambamba na kumpongeza Mama Anne Malecela kwa kuwajibika vyema na kumuhudumia mumewe.
Mwenyekiti Chatanda aliyasema hayo Aprili 21, 2024 wakati wa hafla ya kumpongeza Dkt. John Samwel Malecela kwa kutimiza miaka 90 ya kuzaliwa kwake ambapo Mgeni rasmi wa hafla hiyo alikuwa Dkt Hussein Ali Mwinyi Rais wa Zanzibar, Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi na Makamu Mwenyekiti wa CCM Zanzibar.
Aidha Chatanda , Mary Chatanda , amempongeza Mke wa Waziri Mkuu
Mstaafu Anne Kilango Malecela kwa matunzo na malezi mazuri kwa Mume wake Dkt.
John Samwel Malecela ambaye ameendelea kuwa na afya na siha njema.
"Tunakupongeza Mama Yetu Anna Kilango Malecela kwa kumtunza vizuri mume wako ambaye amelitumikia Taifa ili kwa uzalendo mkubwa katika ngazi mbalimbali," alisema Chatanda.
Katika hafla hiyo pia ilihudhuriwa na viongozi kadhaa wa Seriakali na CCM akiwemo Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara,
Abdulrahman Kinana. 
Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda akizungumza kwenye hafla hiyo.

Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania (UWT) Mary Chatanda, akizungumza na Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara,Abdulrahman Kinana.
Mwenyekiti wa UWT Taifa, Mary Chatanda akionesha furaha yake kwenye hafla hiyo.
Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara,Abdulrahman Kinana. akizungumza kwenye hafla hiyo.
Hafla ikiendelea.
Hafla ikiendelea.
Waziri Mkuu Mstaafu Dkt. John Samwel Malecela akisoma kitabu kwenye hafla hiyo.
Wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo.
No comments:
Post a Comment