Mwenyekiti wa Umoja wa Wanawake Tanzania Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) (kushoto) akiwa kwenye ibada ya kuaga mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti Umoja wa Wanawake Wilaya ya Sengerema Ndg. Jane James Msoga iliyofanyika Mei 3, 2024 katika Kanisa la AICT (African Inland Church Of Tanzania)
..............................
Na Mwandishi Wetu, Mwanza
MWENYEKITI wa Umoja wa Wanawake Tanzania Ndg. Mary Pius Chatanda (MCC) amefika Wilaya ya Sengerema Mkoani Mwanza katika Kanisa la AICT (African Inland Church Of Tanzania) kwaajili ya kushiriki Ibada ya Mazishi ya aliyekuwa Mwenyekiti Umoja wa Wanawake Wilaya ya Sengerema Ndg. Jane James Msoga ambaye alifariki Dunia tarehe 30.04.2024 Katika Hospitali ya Mkoa wa Mwanza Seko Toure.
Mwenyekiti Chatanda akiwa Sengerema amepokelewa na viongozi wa Chama na Serikali wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya Bi. Senyi Ngaga na Kamati ya Ulinzi na Usalama Wilaya, Wajumbe Kamati ya Siasa Wilaya, Wenyeviti wa UWT Wilaya sita za Mwanza.
Marehemu Jane ameacha Mume na Watoto 11 wakiwemo watoto wakike 7 na Wakiume 4. Mwili wake unatarajia kuhifadhiwa katika nyumba yake ya Milele Sengerema Mjini Kata ya Nyampurukano Mei 3, 2024.
Mazishi hayo upande wa Serikali
yameongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Ndg. Said Mtanda na kuhudhuriwa na Wakuu
wa Wilaya Sengerema na Misungwi, Mjumbe Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Viti 20
Tanzania Bara Ndg. Ellen Bogohe, Mwenyekiti CCM Sengerema, viongozi wa UWT Mkoa
wa Shinyanga, Wajumbe Baraza Kuu UWT Taifa, Mbunge Jimbo la Buchosa na
Sengerema, Wabunge Viti Maalum Mkoa wa Mwanza. 



No comments:
Post a Comment